Ushirika

Ümit Girişim Foreign Trade Co… ni kampuni inayofanya biashara ya kimataifa na ina utaalamu wa  kufanya biashara ya bidhaa zenye thamani ya juu. Imeundwa na kampuni sita tofauti kwenye mji  wa Konya nchini Uturuky. Waanzilishi wa Kampuni yetu wana uzoefu wa miaka nyingi katika utengenezaji na  katika ufanyaji biashara ya bidhaa tofauti tofauti kuanzia mashine hadi sekta ya samani.

Kwa ajili ya uzoefu na historia ya biashara ya waundizi wetu,  sisi ni wataalamu wa kutafuta bidhaa bora kabisa kwa bei nafuu. Kwa kuwa na faida hizi na kwa ubora wa huduma wetu, tungependa kukusaidia kuboresha biashara yako. Pia, tuna hamu wa kuwa na uhusiano na wafanyi biashara wapya na wakati huo huo kubaki na mhusiano mwema na wafanyi biashara tuliokuwa na uhusiano tayari.

Kampuni yetu ina muundo imara na inawakilisha nguzo muhimu sana ya biashara ambayo ni uaminifu katika biashara. Utaratibu wa usaidizi kwa wateja baada ya kuuza bidhaa inatolewa na kampuni yetu kama ishara ya maadili ya kibiashara, bei zenye faida kwenye eneo mbali mbali za sekta kwa bidhaa bora zaidi na utengenezaji wenye mwendelezo.

Kampuni yetu inajihusisha katika sekta zifuatazo;

  • Mashine za kilimo na vifaa vya ufugaji wanyama
  • Mashine
  • Samani
  • Mavazi na nguo
  • Viatu
  • Sehemu za magari
  • Vifaa vya kuinua na kusongeza
  • Vifaa vya ujenzi
  • Vifaa na mazao ya kilimo
  • Vifaa vya mahoteli